Go-Suzaku wa Japani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Go-Suzaku (14 Desemba, 1009 – 7 Februari, 1045) alikuwa mfalme mkuu wa 69 (Tenno) wa Japani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Atsunaga, na alikuwa mwana wa Tenno Ichijo. Mwaka wa 1036 alimfuata kaka yake, Tenno Go-Ichijo, na kuwa mfalme hadi kujiuzulu mwaka wa 1045, siku mbili tu kabla ya kifo chake. Aliyemfuata kama Tenno ni mwana wake, Go-Reizei.