Godeleva
From Wikipedia, the free encyclopedia
Godeleva (pia: Godelieve, Godelina; Boulogne, leo nchini Ufaransa, 1052 hivi; Gistel, leo nchini Ubelgiji, 6 Julai 1070) alikuwa mke wa mtu mkatili aliyemtesa sana akishirikiana na mama yake. Hatimaye alinyongwa na wafanyakazi wao wawili kwa sababu alitamani kuwa mtawa kuliko kuolewa[1].
Anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini tangu alipotangazwa na Papa Urbano II mwaka 1084[2].