Gregori wa Narek
From Wikipedia, the free encyclopedia
Gregori wa Narek (kwa Kiarmenia Գրիգոր Նարեկացի, Grigor Narekatsi; 951 hivi - 1003 hivi) alikuwa mmonaki na padri wa Armenia maarufu kama mwanafalsafa, mwanateolojia na mtakatifu wa Kanisa la Kitume la Armenia.
Mzaliwa wa familia ya washairi, akiishi katika monasteri ya Narek (Narekavank), ni "mshairi mkuu wa kwanza wa Armenia".[1]
"Kitabu cha Sala", ambacho pengine kinajulikana kama "Kitabu cha Maombolezo", ni kati ya maandishi bora ya fasihi ya Kiarmenia na kimetafsiriwa katika lugha nyingi.
Papa Fransisko alimtangaza mwalimu wa Kanisa tarehe 12 Aprili 2015.