Hanani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Hanani (kwa Kiebrania חנני, Ḥănānî, maana yake: "YHWH amefadhili"; alizaliwa karne ya 10 KK) alikuwa nabii nchini Israeli katika karne ya 9 KK.
Alikuwa baba wa nabii Yehu na inafikiriwa kwamba waliishi kusini[1] .
Chanzo kikuu cha historia yake ni Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati, sura ya 16[2] .
Kadiri ya kitabu hicho, alimlaumu mfalme wa Yuda Asa kwa kufanya agano na mfalme wa Shamu Ben-Hadad I. Kwa ajili hiyo alifungwa na Asa bila kujali malalamiko ya wafuasi wa nabii huyo.