Hukumu ya mwisho
From Wikipedia, the free encyclopedia
Hukumu ya mwisho, Siku ya hukumu au Siku ya Bwana (kwa Kiebrania "Yohm Ha Din"; kwa Kiarabu يوم القيامة, Yawm al-Qiyāmah au يوم الدين, Yawm ad-Din) ni sehemu ya imani ya dini za Uzoroasta, Uyahudi, Ukristo na Uislamu.
Ni siku ambapo Mungu atahukumu kwa pamoja watu wote walioishi duniani.[1]
Fundisho hilo muhimu lilipewa uzito katika sanaa, hasa ya Kikristo, kwa nyimbo na michoro mbalimbali.