John Bosco
From Wikipedia, the free encyclopedia
John Bosco (16 Agosti 1815 – 31 Januari 1888) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.
Alijitahidi kwa nguvu zake zote kuwalea watoto na vijana, hasa wa kiume, wajifunze kazi na maisha ya Kikristo, akianzisha kwa ajili hiyo Shirika la Mt. Fransisko wa Sales na, kwa kushirikiana na Maria Dominika Mazzarello, “Shirika la Mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo”
Mbinu zake za malezi ni kwa pamoja: akili, dini, hisani. Hakutaka kurekebisha vijana kwa ukali, bali kuwakinga dhidi ya maovu kwa wema. Upendo wake wa ajabu kwa vijana ndio siri ya mafanikio yake ya ajabu katika malezi.
Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 2 Juni 1929 na mtakatifu tarehe 1 Aprili 1934.
Sikukuu yake ni tarehe 31 Januari[1].