Justiniani II
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kaisari Justiniani II (668/669 - 4 Novemba 711) alitawala Dola la Roma Mashariki kuanzia mwaka 685 hadi 695, tena kutoka 705 hadi 711, alipouawa kwa kiburi na ukatili wake.
Alijitahidi kurudisha Dola la Roma katika hadhi yake ya zamani.
Katika historia ya Kanisa anakumbukwa kwa kuendesha mtaguso wa tano-sita katika ikulu yake.
Tangu kale Waorthodoksi wanamheshimu kama mtakatifu.