Kimelea
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimelea (pia: kidusia[1]; kwa Kiingereza parasite) ni kiumbehai ambaye anaishi ndani au juu ya kiumbehai mwingine wa spishi tofauti na kupata virutubishi kutokana na mwili wa kiumbe huyo, ambaye kwa kawaida ni mkubwa zaidi, bila kumpa kiumbe mwenyeji faida yoyote. Kinyume chake, mara nyingi analeta hasara au kusababisha ugonjwa.
Vimelea vingi ni vidogo sana vikiishi ndani ya wanyama au binadamu.