Leah Williamson
mchezaji mpira wa miguu (alizaliwa mwaka 1997) / From Wikipedia, the free encyclopedia
Leah Cathrine Williamson (alizaliwa 29 Machi 1997)[1] ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Uingereza anacheza katika klabu ya Arsenal ya Ligi Kuu ya Wanawake(WSL) na nahodha wa timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza. Mchezaji hodari,mara nyingi akicheza kama beki na pia mara chache kama kiungo.
Pia aliwakilisha timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza kwenye Michezo ya Olimpiki mwaka wa 2021 akiwa nahodha wa Uingereza[2], na aliweza kuisaidia timu yake kutwaa taji la kwanza la kimataifa kwa wanawake, mnamo 2022, ambapo alijumuishwa katika timu ya waliofanya vizuri katika shindano hilo.[3]