Lionel Messi
Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina / From Wikipedia, the free encyclopedia
Lionel Andrés Messi, (matamshi ya Kihispania: [ljonel andɾes mesi]; alizaliwa 24 Juni 1987).Ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Argentina anayecheza katika klabu ya Paris Saint-Germain F.C. (PSG) iliyopo nchini Ufaransa na timu ya taifa ya Argentina.
Mara nyingi huchukuliwa kuwa mchezaji bora wa nyakati zote, Messi kafanikiwa kuchukua tuzo za Ballon d’Or mara tano, kati ya hizo alichukua nne mfululizo, na rekodi ya kunyakua viatu vya dhahabu vya Ulaya mara sita. Maisha yake yote ya soka la kiushindani ameichezea klabu ya Barcelona.[1][2]
Ameshinda mataji 34 yakijumuisha kumi ya La Liga, [[manne ya UEFA Champions League na sita ya Copas del Rey, akiwa mfungaji machachari na kiungo mbunifu, Messi ana Rekodi ya magoli mengi aliyofunga katika La Liga (419), misimu katika soka la ulaya (50) na idadi kubwa ya bao tatu kwa mpigo katika UEFA (8) na idadi kubwa ya pasi za mwisho La Liga (169) na copa America (12). Kwa ujumla kafunga jumla ya magoli 698 katika maisha yake ya kiuchezaji ndani ya klabu na timu ya taifa.[3][4]
Akiwa mzaliwa kutoka katikati ya Argentina, Messi alipata ugonjwa wa homoni ya kukua akiwa mtoto. Alipokuwa na umri wa miaka 13, alihamia Hispania kujiunga na Barcelona, ambao walikubali kulipa matibabu yake. Baada ya mafanikio ya haraka kwenye timu ya watoto ya Barcelona, Messi alicheza mchezo wake wa kwanza wa kiushindani akiwa na umri wa miaka 17 mnamo Oktoba 2004. [5]
Licha ya kuwa katika hatari ya kujeruhiwa wakati wa michezo yake ya awali, alifanikiwa kujijenga kuwa mchezaji muhimu kwa klabu ndani ya miaka mitatu iliyofuata na kufanikiwa kutwaa taji la Ballon d’Or na mchezaji bora wa mwaka wa FIFA wa 2007, na alirudia mwaka uliofuata. Msimu wake wa kwanza bila vikwazo ni wa 2008-2009, ambapo aliisaidia Barcelona kunyakua mataji matatu kwa mpigo katika soka la Hispania.
Akiwa na umri wa miaka 22, Messi alishinda Ballon d'Or na tuzo ya Mchezaji bora wa Mwaka ya FIFA. Misimu mitatu ya mafanikio ilifuatia, Messi akishinda tuzo za FIFA Ballons d'Or mara tautu mfululizo, ikiwa ni pamoja na ya nne ambayo haikukabidhishwa. Katika msimu wa 2011-2012, aliweka rekodi kwenye La Liga kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi ndani ya msimu mmoja, Mnamo Machi 2012 alijitangaza kama mfungaji bora wa wakati wote wa Barcelona.
Kwa misimu miwili iliyofuata, alishika nafasi ya pili kwenye kuwania tuzo za Ballon d’Or nyuma ya mshindani wake mkubwa Cristiano Ronaldo. Messi alirudi kwenye kiwango cha juu msimu wa 2014-2015, na kuvunja rekodi ya magoli mengi kwa msimu mmoja ndani ya La Liga na ligi ya mabingwa ulaya UEFA mwezi Novemba 2014.
Kama mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina, Messi anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wowote wa Argentina. Mwaka 2005, alinyanyua kombe la FIFA mashindano ya vijana, akipata tuzo ya mchezaji bora na mfungaji bora pia, alipata medali ya dhahabu katika mashindano ya olimpiki yam waka 2008. Aina ya uchezaji, kukokota mipira na matumizi ya mguu wa kushoto kulipelekea wengi kumfananisha na mtangulizi wake Diego Maradona, ambaye alimtangaza Messi kuwa mrithi wake. Mchezo wake wa kwanza katika timu ya taifa mnamo Agosti 2005, ulimfanya Messi kuwa mchezaji mdogo zaidi wa Argentina kuwahi kucheza katika mashindano ya Kombe la Dunia ya FIFA katika toleo la 2006, na alifika fainali za Copa América mwaka 2007, ambapo alitwaa tuzo ya mchezaji mdogo wa mashindano hayo. Kama nahodha wa timu ya taifa kutoka Agosti 2011, aliiongoza Argentina kwenye mashindano matatu mfululizo; Kombe la Dunia la mwaka 2014, ambalo alishinda tuzo ya mchezaji bora na Copa América ya mwaka 2015 na 2016. Alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa mwaka 2016 lakini alibadili maamuzi hayo na kusaidia taifa lake kwenye mashindano ya kombe la dunia la FIFA 2018 na kushika nafasi ya tatu katika copa Anmerica ya 2019.
Kulingana na shirika la mpira la Ufaransa, Messi alitajwa kama mchezaji soka anayelipwa ghali Zaidi mwa miaka mitano kati ya sita kuanzia mwaka 2009 hadi 2014, na alitajwa kama mwanamichezo anayelipwa ghali Zaidi na jarida la forbes kwa mwaka 2019. Alikua miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi zaidi kwa miaka ya 2011 na 2012. Messi anafadhiliwa na kampuni ya Adidas inayotengeneza vifaa vya michezo kuanzaia mwaka 2006.