Melissa McCarthy
From Wikipedia, the free encyclopedia
Melissa Ann McCarthy (amezaliwa Agosti 26, 1970)[1] ni mwigizaji filamu, mchekeshaji, mwandishir, na vilevile mtayarishaji kutoka nchini Marekani.
Melissa McCarthy | |
---|---|
McCarthy in September 2014 | |
Amezaliwa | Agosti 26 1970 (1970-08-26) (umri 53) |
Kazi yake | Actress, comedian, writer, producer |
Miaka ya kazi | 1997-hadi sasa |
Ndoa | Ben Falcone (m. 2005–present) «start: (2005-10-08)»"Marriage: Ben Falcone to Melissa McCarthy" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Melissa_McCarthy) |
Watoto | 2 |
Ndugu | Jenny McCarthy (binamu) Joanne McCarthy (binamu) |
McCarthy alianza kupata umaarufu kwa uhusika wake wa Sookie St. James kwenye mfululizo wa TV wa Gilmore Girls (2000–2007). Kwenye ucheshi wa ABC Samantha Who? (2007–2009), amecheza kama Dena. Halafu baadaye akaja kucheza kama Molly Flynn kwenye ucheshi wa CBS Mike & Molly, uhusika ambao umempatia tuzo ya Primetime Emmy Award for Outstanding Lead Actress in a Comedy Series,[2] vilevile kupata kuchaguliwa mara mbili katika mifululizo iliyofuata hapo baadaye.
Vilevile amechaguliwa (bila kushinda) kwa ajili ya tuzo za Primetime Emmy Award for Outstanding Guest Actress in a Comedy Series kwa kazi yake kama mtangazaji wa Saturday Night Live kwa miaka mitatu mfululizo.
McCarthy alianza kupata mafanikio yake makubwa zaidi baada ya kucheza uhusika wake wa Megan Price kwenye filamu ya vichekesho ya mwaka wa 2011 Bridesmaids, ambayo imepelekea kupata kuingizwa katika tuzo kadhaa ikiwa ni pamoja na Academy Award kwa ajili ya Best Supporting Actress, BAFTA na Screen Actors Guild Award zote kwa ajili ya Best Supporting Actress.[3] Mwaka wa 2013, ameshitiki katika filamu ya vichekesho maarufu kama Identity Thief na The Heat. Pia ameonekana katika filamu kama vile The Nines, The Back-up Plan, Life as We Know It and The Hangover Part III. Mwaka wa 2014, McCarthy amecheza katika filamu ya vichekesho Tammy na igizo la St. Vincent.[4] Mwaka wa 2015, amekuwa gumzo katika magazeti mengi duniani kwa kucheza filamu ya mapigano ya Spy. Yeye ndiye mwanzilishi wa kampuni ya filamu ya On the Day Productions akiwa na mumewe Ben Falcone.