Mikoko ni aina za miti au vichaka vinavyokua katika maji ya chumvi kwenye fuko za bahari za kanda za tropiki[1]. Miti hii inaainishwa katika jenasi tatu: Bruguiera, Ceriops na Rhizophora katika familia Rhizophoraceae. Pengine jina hili hutumika kwa Theobroma cacao lakini afadhali jina mkakao litumike kwa mti huu.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Mkoko |
Mkoko magondi (Rhizophora mucronata) |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Plantae (Mimea)
|
(bila tabaka): |
Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
|
(bila tabaka): |
Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
|
(bila tabaka): |
Rosids (Mimea kama mwaridi)
|
Oda: |
Malpighiales (Mimea kama mwenda-usiku)
|
Familia: |
Rhizophoraceae (Mimea iliyo mnasaba na mkoko)
|
Jenasi: |
Bruguiera Savigny
Ceriops Arn.
Rhizophora L.
|
Spishi: |
B. cylindrica (L.) Blume
B. exaristata Ding Hou
B. gymnorhiza (L.) Savigny
B. hainesii C.G.Rogers
B. parviflora (Roxb.) Arn. ex Griff.
C. australis (C.T. White) Ballment & Stoddart
C. decandra (Griff.) W. Theob.
C. pseudodecandra Sheue, H.G. Liu, C.C. Tsai & Y.P. Yang
C. tagal (Perr.) C.B.Rob.
C. zippeliana Blume
R. apiculata Blume
R. x harrisonii Leechm.
R. mangle L.
R. mucronata Lam.
R. racemosa G.Mey.
R. samoensis (Hochr.) Salvoza
R. stylosa Griff.
|
|
Funga
Takriban 1/3 ya pwani kwenye tropiki huwa na mikoko au miti ingine inayoweza kukua katika maji ya chumvi[2]. Msitu wa mikoko huitwa kapa au wangwa.
Mizizi ya mikoko inaweza kushika matope na hivyo husaidia kukinga pwani na kujenga visiwa.