Mpumalanga
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mpumalanga (kabla ya 2002 iliitwa Eastern Transvaal) ni moja kati ya majimbo 9 za Afrika Kusini. Kuna wakazi 3,364,000 (2001) kwenye eno la 79,512 km². Jimbo lilianzishwa mwaka 1994 kutokana na sehemu za jimbo la awali la Transvaal na maeneo ya bantustan KaNgwane, KwaNdebele na Lebowa. Mji mkuu ni Nelspruit.
Mji Mkuu | Nelspruit |
’‘‘Mji Mkubwa’’’ | Nelspruit |
Waziri Mkuu | Thabang Makwetla (ANC) |
Eneo |
Nafasi ya 8 kati ya majimbo ya Afrika Kusini |
- Jumla | 79 490 km² |
Wakazi | Nafasi ya 5 kati ya majimbo ya Afrika Kusini |
- Jumla (2001) | 3 122 994 |
- Msongamano wa watu / km² | 39/km² |
Lugha | SiSwati (30.8%) IsiZulu (26.4%) IsiNdebele (12.1%) Sepedi (10.8%) |
Wakazi kimbari | Waafrika Weusi(92.4%) Wazungu (6.5%) Chotara(0.2%) Wenye asili ya Asia (0.2%) |
Neno Mpumalanga limetokana katika lugha ya Kiswazi likimaanisha "mahali pa macheo".