Nikasi, Eutropia na wenzao
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nikasi, Eutropia na wenzao Fiorenso na Jokundo (walifariki Reims, nchini Ufaransa, 407 hivi) walikuwa askofu wa 10 wa mji huo, dada yake bikira, shemasi na Mkristo mwingine waliouawa na wavamizi Wavandali mbele ya kanisa[1].
Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao ni tarehe 14 Desemba[2].