Notoptera
From Wikipedia, the free encyclopedia
Notoptera (notos = mgongo, ptera = mabawa) ni oda ndogo ya wadudu iliyo na spishi 55 zinazoishi hadi sasa. Spishi hizi zimeainishwa katika familia mbili: Grylloblattidae (wadudu-barafu) na Mantophasmatidae (watambaaji-miamba). Kuna familia mbili za spishi zilizoisha sasa.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Notoptera | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mtambaaji-miamba (Mantophasma zephyra) | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Nusuoda 2 na familia 4:
| ||||||||||||||
Funga
Wadudu-barafu wanatokea Amerika ya Kaskazini na Asia ya Mashariki juu ya milima. Hutafuta arithropodi wadogo waliokufa kwa barafu.
Watambaaji-miamba wanatokea Afrika ya Kusini tu lakini spishi moja inatokea Tanzania. Hula wadudu wengine.