Peter Damian
From Wikipedia, the free encyclopedia
Petro Damiani (Ravenna, Italia, 1007 – Faenza, Italia, 21 Februari 1072) alikuwa mmonaki wa urekebisho wa Wabenedikto wakaapweke wa Camaldoli nchini Italia.
Mmonaki halisi na mwenye msimamo pengine mkali, alitoa ushuhuda wazi wa umuhimu wa kumpa Mungu nafasi ya kwanza na kulenga utakatifu bila kupatana na uovu hata kidogo.
Aliwarudisha wamonaki kwenye madai ya maisha ya sala, waklero kwenye maadili safi na waumini wote kwenye umoja na Papa.
Kutokana na juhudi zake kubwa kwa urekebisho wa Kanisa lote ulioanzishwa na Mapapa wa wakati wake mgumu, alifanywa kardinali askofu na kuwa kati ya watu muhimu zaidi wa karne XI. Athari yake inadumu hata leo katika Kanisa Katoliki.
Tangu zamani ametambuliwa kuwa mtakatifu.
Mwaka 1828 Papa Leo XII alimuongezea sifa ya mwalimu wa Kanisa.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 21 Februari[1].