Pierce Brosnan
From Wikipedia, the free encyclopedia
Pierce Brendan Brosnan (amezaliwa 16 Mei 1953, Drogheda, Ireland) ni mwigizaji filamu na mtaarishaji wa Kiireland-Marekani. Labda anafahamika zaidi kwa kuigiza kama 'James Bond' katika filamu nne alizocheza kuanzia mwaka 1995 hadi 2002, ambazo ni GoldenEye, Tomorrow Never Dies, The World Is Not Enough na Die Another Day. Tangu atumie jina James bond Brosnan, pia amecheza filamu zingine tofauti ikiwemo ile ya "Evelyn" na "Seraphim Falls".
Ukweli wa haraka Amezaliwa, Kazi yake ...
Pierce Brosnan | |
---|---|
Bond kwenye Cannes Film Festival, 2002 | |
Amezaliwa | Pierce Brendan Brosnan 16 Mei 1953 (1953-05-16) (umri 70) Navan, County Meath, Ireland |
Kazi yake | Mwigizaji, mtayarishaji |
Miaka ya kazi | 1979–hadi leo |
Ndoa | Cassandra Harris (1977–1991) (kifo chake) Keely Shaye Smith (2001–hadi leo) |
Tovuti rasmi |
Funga
Pia Brosnan ana kampuni yake inayojishughulisha na maswala ya utengenezaji wa filamu, moja kati ya filamu walizotengeneza ni 'Butterfly on a Wheel, Mamma Mia! na The Topkapi Affair, toka mwaka 1999 alivyo anza ile filamu ya The Thomas Crown Affair.