Pirmini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Pirmini (labda Hispania[1][2][3], 670 hivi[4] - Hornbach, leo nchini Ujerumani, 3 Novemba 753[2] ) alikuwa mmonaki, halafu abati na askofu, tena mmisionari katika maeneo mbalimbali ya Ulaya Kaskazini, alipoanzisha monasteri nyingi [5].
Aliandika pia kitabu cha katekesi "Scarapsus (=Excarpsus) de singulis libris canonicalis" (710-724)[6] .
Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu.