Popo-matunda
From Wikipedia, the free encyclopedia
Popo-matunda ni aina za popo wanaokula matunda hasa. Kibiolojia ni mamalia wa familia ya juu Pteropodoidea katika oda Chiroptera, wanaofanana na panya au mbwa wadogo wenye mabawa. Kwa kawaida spishi hizi ni kubwa kuliko zile za popo-wadudu (oda Yangochiroptera na familia ya juu Rhinolophoidea) lakini kuna spishi zilizo ndogo kulika spishi fulani za popo-wadudu. Yumkini spishi kubwa kabisa ni popo-mbweha wa Uhindi aliye na uzito wa kg 1.6, urefu wa mwili wa sm 40 na urefu wa mabawa wa hadi m 1.5. Mabawa ya popo-mbweha mkubwa yana urefu wa hadi m 1.6. Spishi ndogo kabisa ni popo-matunda mabawa-madoa aliye na uzito wa g 15 na urefu wa mwili wa sm 5-6. Popo-matunda hula matunda au mbochi. Wale wanaokula matunda husambaza spishi za miti na wale wanaokula mbochi huchavusha maua. Kama popo wote hata popo-matunda hukiakia usiko na hulala mchana. Wakilala wananing'inia juu chini na kujifunika kwa mabawa. Takriban spishi zote hulala mitini, lakini spishi kadhaa hulala ndani ya mapango.
Popo-matunda | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Popo mwekundu (Rousettus aegyptiacus) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Nusufamilia 6:
| ||||||||||||||||