Rasi ya Cape York
From Wikipedia, the free encyclopedia
10°41′S 142°32′E Rasi ya Cape York ni rasi kubwa kaskazini mwa jimbo la Queensland, Australia. Ni pori kubwa kabisa la Australia ya mashariki ambayo haina miji na mojawapo ya maeneo ya mwisho ambayo hayajaguswa bado na maendeleo ya kisasa duniani.[1]
Eneo lake ni tambarare bila milima na nusu yake hutumiwa kwa ufugaji wa ng'ombe. Leo hii savana zake za mikalatusi, misitu ya mvua ya kitropiki, na aina nyingine za makazi ya kiekolojia zinatambuliwa kuwa muhimu ulimwenguni. [2]