Remakli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remakli (pia: Remacle, Remaclus, Remaculus, Rimagilus; Aquitaine, leo nchini Ufaransa, karne ya 6 mwishoni au karne ya 7 mwanzoni – Stavelot, leo nchini Ubelgiji, 673 hivi) alikuwa mmonaki padri huko Luxeuil aliyetumwa kuwa abati wa kwanza [1] wa monasteri ya Solignac [2] halafu akakabidhiwa nyingine tatu [3].
Mwaka 650[4] alichaguliwa kuwa askofu wa Maastricht[5]. Hapo kwa miaka kumi na miwili alijitahidi kufanya wakazi Wapagani wa Flandria waongokee Ukristo halafu akarudi monasterini [6][7].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Septemba[8].