Shirakawa wa Japani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Shirakawa (7 Julai, 1053 ā 24 Julai, 1129) alikuwa mfalme mkuu wa 72 (Tenno) wa Japani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Sadahito, na alikuwa mwana wa kwanza wa Tenno Go-Sanjo. Mwaka wa 1073 alimfuata babake, na kuwa mfalme hadi kujiuzulu mwaka wa 1087. Aliyemfuata kama Tenno ni mwana wake, Horikawa.