Sonora (jimbo)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sonora ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kaskazini-magharibi ya nchi. Iko pwani la Ghuba ya California (au Bahari ya Cortez). Mji mkuu na mji mkubwa ni Hermosillo.
Jimbo lina wakazi wapatao 2,394,861 (2005) wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 182,052.
Imepakana na Marekani (Arizona na New Mexico), Chihuahua, Sinaloa na Baja California.
Gavana wa jimbo ni Eduardo Bours Castelo.
Lugha rasmi ni Kihispania.