Arizona
jimbo la Marekani / From Wikipedia, the free encyclopedia
Arizona ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Idadi ya wakazi wa jimbo lote hufikia watu 6,500,180 (2006) wanaokalia eneo la 295,254 km² ambalo sehemu kubwa ni milima na jangwa. Mji mkuu na mji mukubwa jimboni ni Phoenix. Imepakana na Utah, New Mexico (Meksiko Mpya), Mexiko (Sonora na Baja California), California na Nevada. Kuna lugha rasmi 3: Kiingereza (74.1%), Kihispania (19.5%) na Kinavaho (1.9%).