Mtende (mti)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mitende ni miti mikubwa ya jenasi Phoenix katika familia Arecaceae. Matunda huitwa matende.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Mtende (Phoenix dactylifera) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mitende ya kawaida huku Maroko | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Funga
Asili ya miti hii ni ukanda kutoka Visiwa vya Kanari kupitia Afrika ya Kaskazini na Asia ya Kusini mpaka Malaysia na Uchina Kusini.
Mti unaojulikana sana ni mtende wa kawaida na mti huu hupandwa sana katika oasisi za majangwa ya Afrika na Asia na pembezoni kwa majangwa haya.
Mitende ni maarufu katika utamaduni wa Waisraeli na Waarabu. Injili ya Yohane 12:12-19 inataja matawi ya miti hiyo kwamba yalitumika kumshangilia Yesu alipoingia Yerusalemu kwa mara ya mwisho. Ndiyo sababu hadi leo matawi hayo yanatafutwa sana na Wakristo kwa maandamano ya Jumapili ya matawi, wiki moja kabla ya Pasaka.