Spiridoni wa Tremetusia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Spiridoni wa Tremetusia (kwa Kigiriki: Ἅγιος Σπυρίδων; Askeia, Kupro, 270 hivi – Tremetusia 348) alikuwa askofu wa mji huo wa Kupro.
Tangu kale anaheshimiwa na Ukristo wa Mashariki na Ukristo wa Magharibi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa mashariki tarehe 25 Desemba na magharibi tarehe 12 Desemba[1].