Ufalme wa Kongo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ufalme wa Kongo ulikuwa dola la Afrika ya Kati. Eneo lake lilikuwa ndani ya nchi za leo Kongo (Kinshasa), Angola na Kongo (Brazzaville).
Ulianzishwa katika karne ya 14 ikadumu hadi karne ya 17.
Mtawala wake alikuwa na cheo cha "Mwene Kongo" au "Manikongo" wa kabila la Bakongo.
Ufalme huo umejulikana zaidi kihistoria kwa sababu ya mawasiliano yake ya kimataifa. Katika karne ya 15 meli za Wareno zilifika mwambaoni mwake.
Manikongo mbalimbali walijenga uhusiano na Ureno na Kongo ilikuwa taifa la kushikamana na Ureno hadi kuharibika kwa uhusiano huo. Katika kipindi kile taarifa mbalimbali ziliandikwa zinazotupa leo picha nzuri ya ufalme huo.