Uwanja wa Buffalo City
Uwanja wa michezo wa Mji wa Buffalo London Mashariki, Afrika kusini. Hapo mwanzo ulijulikana kama Uwanja wa Ragby. Uwanja huo una uwezo wa kuingiza watu wapatao elfu kumi na sita (16,000). / From Wikipedia, the free encyclopedia
Uwanja wa michezo wa mji wa buffalo ambao hujulikana pia Kama BCM Stadium ni uwanja wa michezo unaopatikana katika nchi ya Afrika Kusini, na mara nyingi hutumika kwa ajili ya michezo ya Rugby na hutumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya Border Bulldogs, ukiwa na uwezo wa kuchukua takribani watu 16,000. Kwa mara kadhaa uwanja huu umekuwa ukibadilishwa jina, jina lake la mwanzo ulikuwa ukijulikana kama Border Rugby Union Grounds, Kwa sababu ya ufadhili, uwanja huu ulibadilishwa jina tena na kuitwa ABSA STADIUM .[1][2] Mnamo tarehe 26 Juni 2010,uwanja huu ulitumika kwa ajili ya mechi za majaribio za timu ya taifa ya Italia na Afrika Kusini na iliibuka na ushindi wa magoli 55 kwa 11.