Vitrisi wa Rouen
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vitrisi wa Rouen (pia: Victricius, Victrice; 330 hivi - 407 hivi) alikuwa askofu wa Rouen, leo nchini Ufaransa, kuanzia mwaka 386 au 393, akafanya umisionari hasa katika maeneo ya Ubelgiji ya leo[1].
Kabla ya kuongokea Ukristo alikuwa askari[2]; baadaye alikataa kuendelea jeshini hata aliteswa sana akahukumiwa kupewa adhabu ya kifo, lakini alifaulu kujinasua.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.