Yohakimu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohakimu (kutoka Kiebrania יְהוֹיָקִים, Yəhôyāqîm, kwa Kigiriki Ἰωακείμ, Iōākeím, yaani "Yule ambaye YHWH amemuinua") anaheshimiwa kama baba wa Bikira Maria na babu wa Yesu kadiri ya mapokeo ya Ukristo na Uislamu, ingawa hatajwi katika Biblia[1] isipokuwa katika kitabu cha karne ya 2 kinachoitwa Injili ya Yakobo na vingine vilivyofuata[2].
Humo anatajwa pia mke wake Ana[3].
Wote wawili wanaheshimiwa kama watakatifu katika madhehebu mengi ya Ukristo, hasa tarehe 26 Julai[4][5].