Zoeradi na Benedikto
From Wikipedia, the free encyclopedia
Zoeradi na Benedikto (karne ya 10 - karne ya 11) walikuwa wakaapweke huko Nitra, leo nchini Slovakia.
Zoeradi (kutoka Opatowiec, Kazimierza, Polandi, mwaka 980 hivi) alipata kuwa mmonaki Mbenedikto kwa jina la Andrea nchini Hungaria, halafu alikubaliwa na abati wa monasteri yake kwenda kuishi upwekeni kama alivyofanya kwanza kwao.
Huko, alipata mfuasi mwenyeji, jina lake Benedikto wa Skalka, akashika pamoja naye maisha magumu sana[1][2].
Papa Gregori VII mwaka 1083 aliwatangaza pamoja kuwa watakatifu.