Inspectah Deck
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jason Hunter (amezaliwa tar. 6 Julai 1970) ni msanii wa muziki wa hip hop, rapa, mtayarishaji, na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Inspectah Deck (pia anajulikana kama Rebel INS). Yeye ni mmoja kati ya wanaounda kundi zima la Wu-Tang Clan. Pia anajulikana kwa staili ya ushairi wake, kwa bahati mbaya, hakuambulia mafanikio mazuri ya kibiashara katika kazi zake za kujitegemea kama jinsi walivyopata wenzi wake kama vile Ghostface Killah au Method Man[1], ingawa bado anaendelea kuheshimiwa na kuendelea kutoa maujanja mapya kibao.
Ukweli wa haraka Maelezo ya awali, Jina la kuzaliwa ...
Inspectah Deck | |
---|---|
Deck, mjini Paris, mnamo 2013 | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Jason Hunter |
Pia anajulikana kama | Rebel INS, Rollie Fingers, Fifth Brother, Ayatollah, Manifesto, Charliehorse |
Amezaliwa | 6 Julai 1970 (1970-07-06) (umri 53) |
Asili yake | The Bronx, New York City, New York |
Aina ya muziki | Hip Hop |
Kazi yake | Rapa, mtayarishaji, mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1989 - hadi sasa |
Studio | Loud, Relativity, Koch, Urban Icon Records |
Ame/Wameshirikiana na | Wu-Tang Clan The Housegang |
Funga