Martha Wang Luoshi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Martha Wang Luoshi (Zunyi, 1812 hivi - Qingyan 29 Julai 1861) alikuwa mwanamke mjane mlei wa China aliyefia Ukristo pamoja na Yosefu Zhang Wenlan, Paulo Chen Changpin na Yohane Mbatizaji Luo Tingyin.
Walifungwa katika handaki lenye joto na unyevu mwingi, waliteswa kikatili na hatimaye walikatwa kichwa[1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[2].