Yosefu Zhang Wenlan
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosefu Zhang Wenlan (1831 hivi - Qingyan 29 Julai 1861) alikuwa mseminari wa China aliyefia Ukristo pamoja na Paulo Chen Changpin, Yohane Mbatizaji Luo Tingyin na Martha Wang Luoshi.
Walifungwa katika handaki lenye joto na unyevu mwingi, waliteswa kikatili na hatimaye walikatwa kichwa[1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[2].