Egidi Maria wa Mt. Yosefu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Egidi Maria wa Mt.Yosefu (Taranto, 16 Novemba 1729 - Napoli 7 Februari 1812), alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Pekupeku kutoka Italia kusini.
Kila siku alikuwa akiombaomba kwa unyenyekevu msaada katika mitaa ya mji akirudisha maneno ya faraja kwa wote.
Jina lake la awali lilikuwa Francesco Antonio Domenico Pasquale Pontillo.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu alipotangazwa na Papa Yohane Paulo II mwaka 1996. Kabla ya hapo alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII mwaka 1888.