Egidi mkaapweke
From Wikipedia, the free encyclopedia
Egidi mkaapweke (kwa Kifaransa: Gilles; 650 hivi – 710 hivi) alikuwa mmonaki Mgiriki[1] kutoka Athens, ingawa habari za maisha yake kiini chake ni mikoa ya Provence na Septimania (leo Ufaransa Kusini).
Inasemekana alianzisha monasteri ambayo ilizaa kijiji kilichopewa jina lake (Saint-Gilles-du-Gard)[2].
Kaburi lake huko limekuwa kituo muhimu cha hija kutoka Arles kwenda Santiago de Compostela kumhesimu mtume Yakobo Mkubwa.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Septemba[3].