Elizabeth I wa Uingereza
Malkia wa Uingereza na Ireland kutoka 1558 hadi 1603 / From Wikipedia, the free encyclopedia
Elizabeth I wa Uingereza (7 Septemba 1533 - 24 Machi 1603) alikuwa malkia wa Uingereza kuanzia 1558 hadi kifo chake. Alikuwa mwanamke wa tatu kutawala Uingereza kama malkia.
Aliitwa mara nyingi "malkia bikira" kwa sababu hakuolewa wala kuzaa watoto. Kutokana na neno la Kiingereza kwa bikira ("virgin") koloni la kwanza la Uingereza likaitwa "Virginia".
Wakati wake ulikuwa kipindi cha kustawi kwa utamaduni na uchumi katika Uingereza ambako William Shakespeare alitunga maigizo na tamthiliya zake, Francis Bacon aliandika falsafa yake na Francis Drake aliweka misingi ya upanuzi wa ukoloni wa Uingereza duniani. Elizabeth alihakikisha pia kipaumbele cha Kanisa Anglikana kama dini rasmi ya taifa na kulitenganisha moja kwa moja na usimamizi wa Papa wa Roma[1].