Henri wa Ufini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Henri wa Ufini (Uingereza, 1100 – ziwa Koylio, Ufini, 20 Januari 1156) alikuwa askofu mmisionari wa Uppsala (Uswidi) kuanzia mwaka 1153.
Alifanya kazi ya kueneza Injili kati ya Wafini hadi alipouawa kikatili na mkulima mzawa ambaye yeye alikuwa amejaribu kumuongoa [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Walutheri na Waanglikana kuwa mtakatifu mfiadini.