Marselino Champagnat
From Wikipedia, the free encyclopedia
Marselino Champagnat (jina kamili kwa Kifaransa: Marcellin Joseph Benedict Champagnat; St. Etienne, Loire, 20 Mei 1789 – Marlhes, 6 Juni 1840) alikuwa padri wa Ufaransa.
Alisaidia kuanzisha Shirika la Maria halafu alianzisha tawi lake kwa mabradha tu ambao wajitose katika malezi ya vijana kulingana na mahitaji ya nchi yake wakati huo.
Siku hizi mabradha hao ni 5,000 hivi na wanaishi katika nchi 74 tofauti.
Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 29 Mei 1955, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 18 Aprili 1999.