Odo wa Cluny
From Wikipedia, the free encyclopedia
Odo wa Cluny (kwa Kifaransa: Odon; Deols, karibu na Le Mans, 880 hivi – 18 Novemba 942) alikuwa abati wa pili wa monasteri ya Cluny.
Aliendeleza urekebisho huo wa Wabenedikto nchini Ufaransa na Italia[1][2].
Habari zake zinapatikana katika kitabu Vita Odonis kilichoandikwa na Yohane wa Salerno, mwanafunzi wake.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake, 18 Novemba[3].