Simeoni wa Mnarani Kijana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Simeoni wa Mnarani Kijana (kwa Kiarabu مار سمعان العمودي الأصغر mār semʻān l-ʻamūdī l-asghar; Antiokia, leo nchini Uturuki, 521 - Antiokia, 24 Mei 592) alikuwa mkaapweke aliyepata umaarufu kwa kuishi miaka 68 juu ya minara mbalimbali akianzia utotoni[1] kwa kufuata mfano wa Yohane, kiongozi wake wa kiroho.
Alipohama mnara mmoja kwenda mwingine alipata nafasi ya kupewa ushemasi halafu upadri.
Mbali na kutenda miujiza mingi, aliacha maandishi mbalimbali[2].
Umeongezewa sifa "kijana" ili kumtofautisha na waliofuata mtindo wake huo kama Simeoni wa Mnarani Mzee, Simeoni wa Mnarani III na Simeoni wa Mnarani wa Lesbos[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Wakatoliki na Waanglikana kama mtakatifu kama mama yake, Marta wa Antiokia.