Yosefu Pignatelli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosefu Maria Pignatelli, S.J. (kwa Kihispania: José María Pignatelli; Zaragoza, Hispania, 27 Desemba 1737 - Roma, Italia, 15 Novemba 1811) alikuwa padri wa Shirika la Yesu aliyeandaa wanashirika kulianzisha upya baada ya kufutwa na serikali.
Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 21 Mei 1933, halafu Papa Pius XII akamtangaza mtakatifu tarehe 12 Mei 1954.