Bundi-panga
Ndege mbuai wa familia Strigidae / From Wikipedia, the free encyclopedia
Bundi-panga ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Surniinae katika familia Strigidae.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Bundi-panga | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Bundi-panga Kaskazi (Surnia ulula) | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Funga
Wengi baina ya ndege hawa wana ukubwa wa bundi, lakini wengine ni wadogo zaidi na wengine wakubwa zaidi.
Wana rangi ya kahawia au kijivu na wengi wana miraba kwa kidari kama vipanga (hii na jinsi yao ya kuwinda ni sababu za jina lao). Spishi ndogo hula wadudu hasa, lakini spishi kubwa huwinda wanyama, ndege na watambaazi pia. Huwinda wakati wa jioni, usiku na alfajiri na pengine mchana. Mara nyingi wamfukuza windo lao kama kipanga.