Ethelreda wa Ely
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ethelreda (pia: Ediltrudis, Editrudis, Audrey; jina asili: Æthelthryth au Æðelþryð au Æþelðryþe; Exning, Suffolk, 636 – Ely, Cambridgeshire, 23 Juni 679) alikuwa mwanamke wa ukoo tawala wa sehemu ya Uingereza aliyeolewa mara mbili na wafalme wa huko kwa sharti la kuachwa bikira.
Hatimaye akawa mmonaki na abesi wa monasteri aliyoianzisha huko Ely, alipolea wanawake wengi kwa mfano wake na mashauri yake[1].
Kama dada zake wote wanne: Etelburga wa Faremoutiers, Vitburga wa Dereham, Seksiburga wa Ely na Setrida wa Faremoutiers anaheshimiwa tangu kale kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana tarehe ya kifo chake[2].