Go-Sanjo wa Japani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Go-Sanjo (3 Septemba, 1034 – 15 Juni, 1073) alikuwa mfalme mkuu wa 71 (Tenno) wa Japani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Takahito, na alikuwa mwana wa pili wa Tenno Go-Suzaku. Mwaka wa 1068 alimfuata kaka yake, Tenno Go-Reizei, na kuwa mfalme hadi kujiuzulu mwaka wa 1073, miezi michache kabla ya kifo chake. Aliyemfuata kama Tenno ni mwana wake, Shirakawa.