Landelini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Landelini (Pas-de-Calais, 625 hivi - Crespin, Hainault, leo nchini Ufaransa, 686 hivi) alikuwa kwanza jambazi kutoka familia tajiri.
Baada ya kuongoka kwa msaada wa Autberi, akawa mmonaki, halafu abati wa monasteri alizoanzisha chini ya kanuni ngumu ya Kolumbani[1] [2][3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[4].