Uislamu huko São Tomé na Príncipe, unakadiriwa kuwa na waumini wapatao 5,500 dhidi ya idadi ya wakazi wote nchini humo ambayo imekadiriwa kuwa 181,000, sawa na asilimia 3 ya wakazi wote wa nchini humo. Asilimia kubwa ya wakazi wa nchini humo ni wafuasi wa Ukristo wa dhehebu la Romani Katoliki ambao wamechukua asilimia 80 ya wakazi wote nchini humo; São Tomé na Príncipe lilikuwa koloni wa Ureno kwa miaka mingi sana, ambao wamekithiri Ukatoliki.[1]
Kuna misikiti na baadhi ya tasisi ambazo zinajiendesha na vilevile zinajulikana nchini humo.[2]